Akaunti ya Kikundi
1. Kujaza fomu ya maombi ya kufungua akaunti ya kikundi (Inapatikana katika Tovuti hii au
Ofisi ya Chama)
2. Muhtasari wa kikao ukionyesha agenda iliyoruhusu kufungua akaunti UVIMA SACCOS
3. Katiba ya kikundi - Kama hakuna katiba, Chama kitasaidia kuandaa kwa gharama nafuu
4. Nakala ya vitambulisho vya watia saini (cha NIDA au namba ya NIDA)
5. Nakala tatu (3) za Passport size kwa watia Saini
6. Kianzio - Fedha angalau Sh. 30,000 kwa ajili ya;
a. Kiingilio Sh. 10,000
b. Kununua Hisa angalau 1 sawa na Sh. 10,000 (Kila mwanakikundi atachangia hisa 1
katika akaunti ya kikundi)
c. Kianzio cha fedha katika akaunti angalau Sh. 10,000 (Akiba/Amana)
7. Kikundi kitatakiwa kuchangia Akiba au Amana isiyopungua Sh. 10,000 kila mwezi
8. Idadi ya chini ya wanachama katika kikundi ili kufungua akaunti ni 5