Maswali yanayoulizwa na wengi…

  • Kujiunga na UVIMA SACCOS ni rahisi kabisa.

    Hatua za kufuata ili kufungua akaunti

    1. Kujaza fomu ya kufungua akaunti (Inapatikana katika Tovuti hii au Ofisi ya Chama)

    2. Passport size 2 za rangi

    3. Kianzio cha fedha cha angalau sh. 30,000

    Akaunti ya Kikundi

    1. Kujaza fomu ya maombi ya kufungua akaunti ya kikundi (Inapatikana katika Tovuti hii au

    Ofisi ya Chama)

    2. Muhtasari wa kikao ukionyesha agenda iliyoruhusu kufungua akaunti UVIMA SACCOS

    3. Katiba ya kikundi - Kama hakuna katiba, Chama kitasaidia kuandaa kwa gharama nafuu

    4. Nakala ya vitambulisho vya watia saini (cha NIDA au namba ya NIDA)

    5. Nakala tatu (3) za Passport size kwa watia Saini

    6. Kianzio - Fedha angalau Sh. 30,000

  • Ofisi yetu inapatikana Mkoa wa Kilimanjaro, Wilaya ya Moshi, Kata ya Marangu Mashariki, Kijiji cha Ashira - Marangu.

    Ofisi ipo katika jengo la KKKT - Ashira Marangu

  • Ndio!

    UVIMA ni Taasisi ya Kifedha inayosimamiwa na wanachama wenyewe ambapo mwanachama ni; mmiliki, mdhibiti/msimamizi na mtumiaji wa huduma zitolewazo na Chama

    UVIMA inasimamiwa na BOT kupitia Tume ya Maendeleo ya Ushirika (TCDC). Usimamizi huu unafuata Misingi ya Ushirika, Sheria ya Vyama vya Ushirika Na. 6 ya 2013 pamoja na Sheria ya Huduma ndogo za Kifedha Na. 10 ya 2018. Hivyo SACCOS hii hukaguliwa kila mwaka na taarifa kuwasilishwa kwa Wanachama ambao ndio wamiliki wa Chama kupitia Mikutano Mikuu.

  • 1.      Atapata semina na mafunzo ya kifedha na kijasiriamali “Bure”

    2.      Atapata gawio la faida katika Hisa, Akiba na Amana

    3.      Fursa ya kuchagua au kuchaguliwa kuwa kiongozi wa Chama

    4.      Kuweka na kutoa fedha bila gharama yeyote

    5.      Kushiriki katika Mikutano Mikuu ya Chama

    6.      Kuitisha Mkutano Mkuu kulingana na Kanuni

    7.      Kukopa kulingana na taratibu za Chama ambapo Chama chetu hutoa mikopo kwa kuzingatia dhamana za kawaida ambazo ni rahisi na zinapatikana katika mazingira yetu.

    8.      Kupatiwa habari za Chama, Kusikilizwa na Kutoa Maoni katika Chama

  • Ushirika ni Biashara

    Ushirika ni Uhiari (Mungano wa Uhiari)

  • Watu walioungana pamoja kwa HIARI yao ili kuweka fedha zao pamoja na kukopeshana kwa lengo la kujiendeleza kiuchumi, kiutamaduni na kijamii.

    SACCOS ni kifupisho cha neno la Kingereza likiwa na maana ya “Savings and Credit Co-operative Society” ikiwa na maana ni aina ya Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo.

    SACCOS ni Taasisi ya fedha inayoanzishwa na watu kwa ajili ya kuwawezesha kupata huduma za kifedha kwa lengo la kujiendeleza kiuchumi na kijamii.

    SACCOS inaandikishwa, kuendeshwa na kusimamiwa kwa mujibu wa Sheria ya Vyama vya Ushirika, Kanuni, Sheria za fedha, Masharti ya Chama na Sera/miongozo mbalimbali

  • Ndio. UVIMA kama Chama chochote cha Ushirika ambacho madhumuni yake ni kuinua hali ya kiuchumi ya wanachama wake kinafuata misingi ya uendeshaji na usimamizi wa shughuli za ushirika. (Tazama misingi ya Ushirika hapa)