Maswala ya Uanachama
Je, unapenda kuwa mwanachama ili kumiliki SACCOS yako, tafadhali bofya kitufe hapo chini kupakua (download) fomu, ijaze na kisha iwasilishe kupitia njia zifuatazo;
Ofisi ya UVIMA - Siku za kazi
Tuma maombi kupitia Barua Pepe (Email)
Tuma kwa njia ya Simu (WhatsApp)
-
Kwa mujibu wa Sheria, Mwanachama mwenye hisa kamili ndiye mmiliki halali wa SACCOS na ndiye
anayeendesha SACCOS.
Katika UVIMA SACCOS mwanachama ana nafasi zifuatazo:
Mmiliki: Kwa kuwa amenunua hisa za chama
Mteja: Hutumia huduma za chama
Mshirika wa mgao: Hushiriki mgawanyo wa ziada kwa jinsi alivyochangia kuzalisha ziada hiyo
Kiongozi: Anayo haki ya kuchagua viongozi au kuchaguliwa kuwa kiongozi
-
Mtu yeyote anaweza kuwa mwanachama endapo atakidhi mahitaji ya Fungamano la pamoja la uanachama na sharti awe na sifa zifuatazo: -
1. Umri wa miaka isiyopungua 18
2. Awe mtu binafsi au kikundi cha VICOBA/Kijasiriamali na anayepatikana ndani ya wilaya ya Moshi vijijini.
3. Awe na uwezo wa kulipa kiingilio, hisa za uanachama na ... soma zaidi
-
HAKI ZA MWANACHAMA (Mwanachama atanufaika nini?)
1. Atapata semina na mafunzo “Bure”
2. Atapata gawio la faida katika Hisa, Akiba na Amana
3. Fursa ya kuchaguliwa kuwa kiongozi wa Chama
4. Kuweka na kutoa fedha bila gharama yeyote …Soma Zaidi
WAJIBU WA MWANACHAMA
1. Kukamilisha kununua hisa na kuweka akiba kwa kuzingatia Masharti ya chama.
2. Kurejesha mkopo kwa wakati uliopangwa;
3. Kuteua Mrithi - Mwanachama atamteua mrithi wake ambaye atakuwa na haki ya kulipwa
hisa au maslahi mengine katika Chama.
4. Kumdhamini mkopo mwanachama mwenzake … Soma Zaidi
-
Ili kufungua Akaunti UVIMA SACCOS unatakiwa kufanya yafuatayo;
Akaunti ya mtu Binafsi
1. Kujaza fomu ya kufungua akaunti (Inapatikana katika Tovuti hii au Ofisi ya Chama)
2. Passport size 2 za rangi
3. Kianzio cha fedha cha angalau sh. 30,000... Soma Zaidi
Akaunti ya Kikundi
1. Kujaza fomu ya maombi ya kufungua akaunti ya kikundi (Inapatikana katika Tovuti hii au
Ofisi ya Chama)
2. Muhtasari wa kikao ukionyesha agenda iliyoruhusu kufungua akaunti UVIMA SACCOS
3. Katiba ya kikundi - Kama hakuna katiba, Chama kitasaidia kuandaa kwa gharama nafuu
4. Nakala ya vitambulisho vya watia saini (cha NIDA au namba ya NIDA)
5. Nakala tatu (3) za Passport size kwa watia Saini
6. Kianzio - Fedha angalau Sh. 30,000... Soma Zaidi
Bonyeza kitufe hapo Chini Kupakua (DOWNLOAD) Fomu ya kufungua Akaunti UVIMA SACCOS LTD