HUDUMA NYINGINEZO ZITOLEWAZO NA CHAMA

Huduma 1: Uhamasishaji na Ukusanywaji wa Hisa, Akiba na Amana

Hisa ni nini?

  • Hisa ni mtaji wa Chama na ndio inayompa uwezo mwanachama kuwa mmiliki halali wa Chama

  • Thamani ya Hisa moja ni Sh 10,000 na mwanachama atatakiwa kulipa kiwango cha chini cha hisa ishirini (20) ndani ya kipindi kisichozidi mwaka mmoja ambazo ni sawa na Sh. 200,000.

  • Kima cha juu cha Hisa ni 50 sawa na Sh. 500,000

  • Endapo mwanachama atakoma uanachama anaweza kuuza hisa zake ama kuzichukua kwa muda usiozidi siku tisini (90) kama hatakuwa na deni lolote chamani.

  • Kiwango cha hisa chaweza kushuka au kupanda kulingana na maamuzi ya Mkutano Mkuu.

  • Hisa italipiwa Gawio kila mwaka pale Chama kinapopata faida.

Akiba ni nini?

  • Hii ni fedha anayoweka mwanachama kwa malengo ya baadae

  • Akiba inaweza kutumiaka kama sehemu ya dhamana ya mkopo

  • Mwanachama anahimizwa kujiwekea akiba isiyopungua shilingi elfu kumi (10,000) kila mwezi na kuendelea kudumisha uhai wake katika chama.

 

Amana ni nini?

  • Amana ni fedha inayowekwa kwa ajili ya dharura

  • Mwanachama anaweza kuchukua amana yake muda wowote

  • Kima cha chini cha Amana itakayowekewa faida ni Sh. 50,000

  • Kima cha chini cha baki ya Amana katika akaunti ni Sh. 10,000

  • Amana ya muda maalumu itatengewa faida ya hadi asilimia 6%. Na ni ile iliyokaa chamani zaidi ya miezi sita.

Huduma 2: Elimu juu ya Utunzaji wa Mazingira

Kwa kushirikiana na Vikundi na wadau mbalimbali tunahamasisha utunzaji wa Mazingira (Aidha katika hili, Tunawahamasisha wanachama na jamii kutumia taa za sola, majiko banifu pamoja na kutengeneza mitambo ya Biogas inayotumia kinyesi cha wanyama jambo ambalo limepunguza matumizi ya kuni kwa kiasi kikubwa.)

Huduma 3: Uhamasishaji na Usimamizi wa Vikundi Biashara na VICOBA

Chama kina Kibali cha uhamasishaji wa Biashara ya Huduma ndogo za Fedha

Kibali hiki hutolewa na Halmashauri ya Wilaya Chini ya Kanuni ya 16(2) ya Kanuni za Huduma Ndogo za Fedha (Majukumu ya Waziri) ya mwaka 2019 ili kutoa huduma za uhamasishaji zilizoruhusiwa kwa mujibu wa sheria.

Kibali hiki kinalenga Uhamasishaji na Usimamizi wa vikundi vya Kijasiriamali

Huduma 4: Elimu na Mafunzo juu ya Kilimo Hai

Mafunzo haya ya kijasiriamali kwa wanachama hutolewa bure ambapo hujumuisha utoaji wa elimu juu ya kilimo hai kisichotumia madawa na mbolea zenye kemikali

Huduma 5: Mafunzo kwa wanachama, watendaji na viongozi

Chama kimekua kikitoa elimu na mafunzo kwa wanachama, viongozi, na watumishi ili waweze kuchangia kikamilifu katika maendeleo ya chama chetu. Hii inajumuisha utoaji wa habari kuhusu kuwepo, na manufaa ya ushirika (SACCOS) kwa jamii hususani vijana na viongozi wa serikali, dini, kimila, vyama vya siasa.