Lengo Kuu la Mkopo

Ni kumwezesha Mwanachama kupata Ustawi wa Kiuchumi, Kijamii na kiutamaduni.

Mikopo hutolewa kwa wanachama (ikiwemo kikundi mwanachama) waliotimiza vigezo pekee

    1. Mikopo hutotewa kwa kigezo kisichozidi mara tatu ya akiba ya mwanachama

    2. Tangu chama kianzishwe mwaka 2007 hadi sasa kimekua kikitoa mikopo kwa kutumia mtaji wa ndani (Hatujawahi kukopa nje)

    3. Mikopo hutolewa kwa wanachama (ikiwemo kikundi mwanachama) waliotimiza vigezo pekee

    4. Mkopo hutolewa kwa mwanachama baada ya siku 90 tangu mwanachama huyo ajiunge na SACCOS 

    5. Mwanachama ambaye anaruhusiwa kupata mkopo ni yule ambaye atakuwa tayari ameshalipa agalau Hisa 10 na kujiwekea akiba ambayo ndio mtaji wa kukopea.

    6. Chama hutoa mikopo ya hadi Shilingi Milioni 20 (Sh. 20,000,000/=)

    7. Chama hutoa msamaha wa riba kwa muda wa mwezi mmoja kama motisha ili mkopaji ajipange kuanza marejesho (Grace Period)

  • Chama kinatoa mikopo kwa ajili ya Biashara, Elimu, Kilimo, Ufugaji, Ujenzi na Vikundi

    1. Fomu hizi zinapatikana Ukurasa wa mbele wa Tovuti hii au tutembelee Ofisi ya UVIMA SACCOS iliyopo KKKT, Usharika wa Ashira Marangu, Chumba Na. 13

    2. Tafadhali pakua/download fomu ya maombi ya mkopo, kisha ijaze na kuirudisha ofisi ya UVIMA au itume kupitia WhatsApp Na. 0658125954 au Barua Pepe - uvimasaccos@gmail.com

    1. Mikopo ya Biashara, Elimu, Ufugaji na Kilimo hutolewa kwa riba ya 18%. Muda wa juu wa mikopo hii ni mwaka 1 (Miezi 12)

    2. Mikopo ya Ujenzi hutolewa kwa riba ya 18%. Muda wa juu wa mikopo hii ni miaka 2 (Miezi 24)

    3. Mikopo maalumu kwa ajili ya Wajane na Walemavu hutolewa kwa riba ya 15%. Muda wa juu wa mikopo hii ni miaka 2 (Miezi 24)

    4. Mkopo wa Dharura unatolewa kwa riba ya 5% kwa Muda wa Mwezi 1 tu.

    5. Kiwango cha juu cha Mkopo ni Sh. 20,000,000

    6. Mkopaji atatakiwa kununua fomu ya mkopo pamoja na kulipia gharama za bima.