Upekee wa UVIMA SACCOS LTD

Upekee wa UVIMA SACCOS LTD ☆

Hii ni SACCOS ya kipekee Tanzania iliyoanzishwa baada ya vikundi vya VICOBA kuungana kwa lengo la kukuza mtaji wa Pamoja.

Upekee wa SACCOS hii unadhihirishwa kwa namna inavyojiendesha kwa kufuata Dhana ya Ushirika

Dhana ya Ushirika

  • Maana ya Ushirika – Uhiari (Muungano wa Uhiari)

  • Maana ya Ushirika wa Akiba na Mikopo (SACCOS) – Ni watu walioungana pamoja kwa HIARI YAO ili kuweka fedha zao pamoja na kukopeshana kwa lengo la kujiendeleza kiuchumi, kiutamaduni na kijamii.

  • Ukepee wa Ushirika (UVIMA) - Ni Biashara inayosimamiwa na wanachama wenyewe ambapo mwanachama ni; mmiliki, mdhibiti/msimamizi na mtumiaji wa huduma zitolewazoz na Chama.

TUNAJIVUNIA ZAIDI YA MIAKA 16 YA MAFANIKIO KWA KUTOA HUDUMA BORA KWA JAMII

Mafanikio hayo ni pamoja na;

  • Kwa miaka 16 (Kuanzia 2008 hadi Juni 2024) Chama kwa kutumia mtaji wa ndani kimefanikiwa kutoa huduma za mikopo kwa wakati kwa Wanachama wake wote waliotimiza vigezo na masharti bila kukopa nje.

     

    Jumla ya Mikopo iliyotolewa ni Sh. ……….

    Na iliyorejeshwa Sh. …………

  • Chama kinamiliki Mfumo wa utunzaji wa Taarifa ili kurahisisha uchakatwaji wa taarifa mbalimbali na kutoa ripoti kwa wakati.

  • Kwa miaka 16 Chama kimeendelea kukaguliwa kwa wakati na Shirika la Wakaguzi wa Kimataifa COASCO

  • Chama kina leseni ya kutolea huduma kwa mujibu wa Sheria ya Huduma ndogo ya Fedha Na. 10 ya 2018

    Leseni yetu ni Daraja A - Leseni Na. MSP3-TCDC/2023/00333

  • Kibali hiki hutolewa na Halmashauri ya Wilaya Chini ya Kanuni ya 16(2) ya Kanuni za Huduma Ndogo za Fedha (Majukumu ya Waziri) ya mwaka 2019 ili kutoa huduma za uhamasishaji zilizoruhusiwa kwa mujibu wa sheria.

    Kibali hiki kinalenga Uhamasishaji na Usimamizi wa vikundi vya Kijasiriamali

    • Kufanyika kwa Mikutano Mikuu na Mikutano Maalumu ya Chama kwa Wakati

    • Hakuna Makato katika Akaunti zetu

    • Chama hutoa Punguzo la Riba kwa Wajane na Walemavu

UVIMA DAY

Karibu utazame habari picha kuhusiana na matukio ya

UVIMA DAY

UVIMA DAY ni nini?

UVIMA Day ni maonyesho ya UVIMA yaliyoandaliwa na UVIMA SACCOS kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ambao ni marafiki wa UVIMA na ambayo huleta kwa pamoja shughuli  mbalimbali zinazofanywa na wanachama/wateja wa UVIMA SACCOS ili  kuelezea jamii na umma wa Watanzania kwa ujumla juu ya mafanikio waliyoyapata na faida za kujiunga kwenye Ushirika yaani SACCOS Yetu.

Hakika kwa kupitia UVIMA DAY wanachama wetu wanajivumia kuwa na SACCOS hii ya kijamii kwani wamenufaika sana kwa mambo mengi ikiwemo Mikopo ya kilimo, ufugaji, biashara pamoja na mafunzo ya kilimo na ujasiriamali bure.

Kutokana na umuhimu wa maonyesho haya, Bodi ya uongozi ilipendekeza siku hii kuazimishwa kila mwaka na kilele chake kuwa ni Wiki ya mwisho ya mwezi Septemba ya kila mwaka ambayo ndiyo Birth Day ya UVIMA SACCOS LTD.

UVIMA DAY 2018

  • Mchg. Humphrey Mboya

    Aliyekua Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto; Dr. Faustine Ndugulile (Mb) akipokea maelezo toka kwa aliyekua mwenyekiti wa Bodi ya UVIMA (2021 - 2023) Mchg. Humphrey Mboya, kuhusiana na faida aliyopata (Mwenyekiti wa UVIMA) kutokana na ufugaji wa mbuzi wa maziwa alipotembelea Maonyesho ya UVIMA DAY 24/11/2018. Kupitia maonyesho haya, Naibu alikubali kazi za UVIMA hasa shughuli zinazofanywa na Chama kuhusiana na maswala ya kuweka na kukopa, elimu juu ya ufugaji, kilimo hai na utunzaji wa mazingira.

  • Mama Madona G. Ngowi

    Madona G. Ngowi ambaye ni Mwanachama wa UVIMA na mfanya biashara maarufu katika Masoko ya Himo, Marangu na Mwika akimwelezea aliyekuwa Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto; Dr. Faustine Ndugulile (Mb) faida aliyoipata UVIMA na namna Chama kilivyomwezesha katika biashara yake ya mbogamboga na matunda. Aliyesimama kushoto ni Mkurugenzi wa Shirika la Floresta (Ndugu Richard Mhina)

    “Kupitia UVIMA SACCOS, mbali na kufanikiwa katika biashara, pia nilifanikiwa kuwasomesha Watoto wangu wawili nje ya Nchi pamoja na kujenga nyumba bora ya kuishi” Alisema Madona

  • Mr. Jackson Mtui

    Meneja wa UVIMA SACCOS LTD (Ndugu Jackson Mtui) akitoa maelezo ya kina kwa Mgeni rasmi aliyekuwa Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto; Dr. Faustine Ndugulile (Mb) wakati wa maonyesho ya UVIMA DAY juu ya bidhaa za Sola ambazo hutolewa kama huduma kwa wanachama na jamii ili kuhamasisha utunzaji wa Mazingira. UVIMA SACCOS ilipata tuzo kama Mshindi Na. 1 katika uhamasishaji wa Nishati Mbadala kupitia kampeni ya Hamia Nishati Safi na Salama Sasa iliyoendeshwa na Shirika la SNV Arusha.

    Aliyesimama kulia ni Mchg. Winford Mosha (Mwenyekiti wa Floresta TZ) na Kushoto ni ndugu Richard Mhina (Mkurugenzi wa Floresta Tz)