HABARI MPYA ZILIZOJIRI KARIBUNI

Mkutano Mkuu wa 17 wa UVIMA

Ripoti na Takwimu

Maktaba ya Picha

Maktaba ya Video

Bofya hapa kujishindia

Zawadi mbalimbali

Download hapa Fomu ya

Shindano la Zawadi

Wasiliana nasi ili kujipatia NAKALA YAKO ya Kitabu cha Mkutano Mkuu hapa Chini (Kwa wanachama wa UVIMA pekee)

Bofya kitufe hapo chini kutuma maoni, maswali, ushauri, pongezi au maombi ya nakala ya kitabu cha Mkutano Mkuu wa 17 wa UVIMA SACCOS LTD

MADHUMUNI YA UVIMA SACCOS

Kuondoa umaskini na kukuza kipato kwa kuinua, kuimarisha na kuendeleza hali ya kiuchumi na kijamii ya wanachama wake kwa kufuata Sheria, Kanuni na taratibu za Vyama vya Ushirika.

Aidha, Shughuli za msingi kwa UVIMA ni kuhimiza uwekaji wa fedha ambao ni akiba (savings) na upatikanaji wa mikopo kwa wanachama na wazalishaji wadogo.

Eneo la Shughuli za UVIMA SACCOS

Ni Tanzania Bara hususani katika Mkoa wa Kilimanjaro, ndani ya Wilaya ya Moshi

 

WASIFU WETU

Dhima (Mission)

Kuwa chama imara cha Ushirika chenye kutoa huduma bora za kifedha ili kuboresha maisha ya jamii Masikini iishiyo vijijini.

Dira/Njozi Yetu (Our Vision)

Kuwa taasisi bora ya kifedha inayoboresha maisha ya jamii masikini iishiyo vijijini kwa kufanya yafuatayo;

  • Kutoa elimu ya ushirika kwa wananchi ili waweze kujiunga kwenye SACCOS yetu ya UVIMA.

  • Kutoa elimu ya ujasiriamali kwa vikundi na wanachama ili waweze kutumia fursa zilizopo na kujikomboa na umasikini

Lengo kuu (Main Objective)

Lengo kuu ambalo chama kinatarajia kufikia ifikapo mwishoni mwa 2025 ni kuwa na mtaji unaotosheleza mahitaji ya mikopo ya wanachama.

Malengo mengine ni Pamoja na;

  • Kuwezesha Wanachama wake kuweka akiba na kukopa mikopo kwa Masharti nafuu kabisa.

  • Kuviunganisha Vikundi vya VICOBA, vikundi vya Wajasiriamali na Wanachama wake na kuvisimamia.

UJUMBE MAALUMU TOKA KWA MENEJA 2024

Jackson Mtui - Meneja

Jackson Mtui

Meneja

Tuamshukuru sana Mungu kwa kutuwezesha Kufanya Mkutano Mkuu wa 17 tarehe 20 Nov. 2024. Mkutano huu uliambatana na Uzinduzi wa Tovuti hii pamoja na Mobile App.

Mgeni Rasmi katika Mkutano huu alikuma Mama Edith Banzi ambaye ni mwanzilishi wa SACCOS hii (wakati akiwa Mkurugenzi wa Shirika la Floresta Tz 2004 - 2011)

Pia kupitia Mkutano huu, Chama kilitoa Cheti cha Pongezi na zawadi kwa Mwakachama Bora wa SACCOS... Soma zaidi kuhusu Mkutano Mkuu wa 17 wa UVIMA

TULIPOTOKA

Hapo awali SACCOS hii ilikuwa ikihudumia wanachama waliounganishwa kupitia vikundi vya Kijasiriamali ikiwemo VICOBA. Kutokana na mtaji wa Chama kukua, pamoja na mahitaji makubwa ya huduma za kifedha katika jamii inayotuzunguka, Chama kilifikia wakati wa kufanya mabadiliko ya Kisera, Masharti na miongozo mbalimbali ili kupanua wigo na fungamano letu na hatimaye kuweza kuhudumia wanachama nje ya vikundi. Hivyo kwa sasa UVIMA SACCOS inapokea na kuhudumia mtu yeyote atakayekidhi vigezo vya fungamano letu.

Kwa undani zaidi juu ya SACCOS hii, tafadhali nakukaribishwa kwa moyo wa ukunjufu kutembelea tovuti hii kwani utaweza kupata uelewa zaidi juu ya... Soma Zaidi

HATI ZA UTAMBULISHO

UVIMA SACCOS LTD

SACCOS ya Kijamii      -           Daraja A

Nambari ya Usajili

Usajili wa zamani - Na. KLR 712

Usajili mpya - Na. PRI-KJR-MSH-DC-2022-1427 

Nambari ya Leseni 

Leseni ya Zamani - Na. MSP3-TCDC-2021-00304

Leseni Mpya - Na. MSP3-TCDC-2023-00333

TRA TIN Na. - 142-184-079