UJUMBE MAALUMU TOKA KWA MENEJA 23/09/2024

UVIMA ni Taasisi ya Kifedha iliyoanzishwa mwaka 2007

Wakati Chama kikijiandaa kufanya Mkutano wake Mkuu wa Mwaka wa 17 (Nov. 2024), mwaka wetu wa fedha unakaribia kumalizika ambapo SACCOS hii imetimiza miaka 17.

Hapo awali SACCOS hii ilikuwa ikihudumia wanachama waliounganishwa kupitia vikundi vya Kijasiriamali ikiwemo VICOBA. Kutokana na mtaji wa Chama kukua, pamoja na mahitaji makubwa ya huduma za kifedha katika jamii inayotuzunguka, Chama kilifikia wakati wa kufanya mabadiliko ya Kisera, Masharti na miongozo mbalimbali ili kupanua wigo na fungamano letu na hatimaye kuweza kuhudumia wanachama nje ya vikundi. Hivyo kwa sasa UVIMA SACCOS inapokea na kuhudumia mtu yeyote atakayekidhi vigezo vya fungamano letu.

Kwa undani zaidi juu ya SACCOS hii, tafadhali nakukaribisha kwa moyo mkunjufu kutembelea tovuti hii kwani utaweza kupata uelewa zaidi juu ya;

1.       Historia fupi ya UVIMA SACCOS (UVIMA maana yake nini?)

2.       Wasifu wa Chama

3.       Wanachama (aina mbalimbali za Wanachama/Akaunti za SACCOS)

4.       Huduma na bidhaa zitolewazo na Chama

5.       Sifa, haki, wajibu na ukomo wa mwanachama

6.       Mafanikio ya Chama

7.       Dhana na Historia ya Ushirika (SACCOS)

8.       Wadau wa Ushirika (SACCOS) – Tanzania

 

Kauli Mbiu ya Chama UVIMA SACCOS ndio mkombozi wetu, huondoa umasikini na kuboresha mazingira yetu”