Sisi UVIMA SACCOS ni nani?
UVIMA ni kifupi cha maneno - Umoja wa VICOBA Marangu
Hiki ni Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo kilichoanzishwa tarehe 05/09/2007 baada ya wanachama waliokua ndani ya vikundi vya VICOBA kuungana na kuanzisha SACCOS
Kwa sasa UVIMA SACCOS LTD inahudumia mtu yeyote hata kama sio mwanakikundi wa VICOBA ili mradi akidhi hitaji la fungamano letu.
Mwaka wa Fedha wa Chama unaanzia Januari 01 hadi Desemba 31 ya kila mwaka husika
-
Ni Mfungamano wa pamoja wa Wanachama wa UVIMA wanaopatikana ndani ya Wilaya ya Moshi ikiwemo vikundi na watu binafsi ambao wengi wao ni wafanyakazi, wakulima, wafugaji na wafanyabiashara wadogo wadogo.
-
Kuondoa umaskini na kukuza kipato cha Wanachama kwa kufuata Sheria, Kanuni na taratibu za Vyama vya Ushirika.
Aidha, Shughuli za msingi kwa UVIMA ni kuhimiza uwekaji wa fedha na upatikanaji wa mikopo kwa wanachama na wazalishaji
-
Kuwa Chama imara cha Ushirika chenye kutoa huduma bora za kifedha ili kuboresha maisha ya jamii Masikini iishiyo vijijini.
-
Kuwa taasisi bora ya kifedha inayoboresha maisha ya jamii masikini iishiyo vijijini kwa kufanya yafuatayo;
Kutoa elimu ya ushirika kwa wananchi ili waweze kujiunga kwenye SACCOS yetu ya UVIMA
Kutoa elimu ya ujasiriamali kwa vikundi na wanachama ili waweze kutumia fursa zilizopo na kujikomboa na umasikini
-
Lengo kuu ambalo chama kinatarajia kufikia ifikapo mwishoni mwa 2025 ni kuwa na mtaji unaotosheleza mahitaji ya mikopo ya wanachama
Malengo mengine ni pamoja na;
Kuwezesha wanachama wake kuweka akiba na kukopa mikopo kwa masharti nafuu kabisa
Kuviunganisha vikundi vya VICOBA, vikundi vya wajasiriamali na wanachama wake na kuvisimamia
-
Kila wakati chama hufanya mabadiliko katika uongozi wake kulingana na Sheria ya Vyama vya Ushirika ya kipindi husika.
Uongozi uliopo madarakani ulichaguliwa mnamo mwezi Machi 2024 na utadumu kwa kipindi cha miaka 3
Wajibu wa Uongozi umeainishwa ndani ya ukurasa huu
-
Takwimu hizi zinaonyesha tathinini ya hali ya ukuaji wa chama kwa kipindi cha miaka 3 iliyopita.
Bonyeza kitufe hapo chini kutazama takwimu za Chama
Muundo wa Chama
UVIMA SACCOS LTD
☆
Muundo wa Chama UVIMA SACCOS LTD ☆
MWANACHAMA
Mwanachama mwenye hisa kamili ndiye mmiliki halali wa SACCOS na ndiye anayeendesha Chama (Kupitia Mikutano Mkuu)
Pia Mwanachama ana haki ya kushiriki katika Uongozi (Kuchagua au kuchaguliwa)
BODI YA CHAMA
Mungubariki J. Tarimo MWENYEKITI WA BODI
Wajibu wa Bodi
Kwa mujibu wa Sheria Bodi ya Uongozi wa Chama inatakiwa kuwa na wajumbe wasiopungua watano (5) na wasiozidi tisa (9) akiwemo mwenyekiti na makamu wake.
Wajibu wa Bodi ni kusimamia shughuli zote za utendaji wa chama ikiwemo;
Kuajiri na kuteua watumishi wenye sifa za kutosha kutenda shughuli za Chama wakiwemo Meneja, Mhasibu, Mweka Hazina au watumishi wengine ambao wataendesha shughuli za kila siku za chama
Kuingia mikataba mbalimbali kwa niaba ya chama kwa kuzingatia Kanuni za Vyama vya Ushirika;
Msemaji wa Bodi/Chama:
Mwenyekiti ndiye msemaji mkuu wa chama.
WAJUMBE WENGINE WA BODI
-
Samwel Ch. Mosha
Makamu Mwenyekiti
-
Mthiolojia Cuthbert N. Moshi
Mjumbe
-
Safinaeli M. Tarimo
Mjumbe
-
Jackson S. Shayo
Mjumbe
KAMATI YA USIMAMIZI
Wajibu wake ni kukagua shughuli za SACCOS na kujiridhisha kuwa SACCOS inaendeshwa kwa mujibu wa sheria, masharti, sera na maazimio mbalimbali ya Mikutano Mikuu
WAJUMBE WA KAMATI YA USIMAMIZI
-
Eldavis Salvatory Elihuruma
Mwenyekiti
-
Rogathe Robert Minja
Katibu
-
Rogathe August Minja
Mjumbe
WAFANYAKAZI
-
JACKSON MTUI
Meneja
-
GODLISTEN M. SHAO
Mhasibu
-
Hosiana G. Urio
Karani
-
Jackline E. Mshanga
Afisa Mikopo
-
JACKLINE S. MWANGA
Afisa Mikopo
-
EMANUEL MOTTEY
Afisa Masoko