Takwimu za UVIMA SACCOS LTD
Takwimu hizi zinaonyesha tathimini ya hali ya ukuaji wa Chama kwa kipindi cha Miaka 4 mfululizo
UVIMA ni nini?
UVIMA ni kifupi cha maneno (Umoja wa Vikundi Marangu)
Hiki ni Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo kilichoanzishwa na kusajiliwa tarehe 05/09/2007. Chama hiki kilipewa namba ya usajili KLR 712 chini ya Sheria ya Vyama vya Ushirika Na. 20 ya 2003
Mnamo mwaka 2022 UVIMA SACCOS ilipata usajili mpya Na. PRI-KJR-MSH-DC-2022- 1427
Aidha, mnamo tarehe 04/07/2023 UVIMA ilipata Leseni mpya ya kutolea huduma ndogo za kifedha; Leseni Na. MSP3-TCDC-2023-0033. Leseni hii ilitolewa chini ya kifungu cha 20 cha Sheria ya Huduma Ndogo za Kifedha Na. 10 ya mwaka 2018 baada ya Chama kutimiza matakwa yote ya Kisheria.
HISA
AKIBA
WANACHAMA
Miongoni mwa sababu ambazo zimesaidia chama kufanya vyema ni;
Mahusiano mazuri baina ya Mwajiri/viongozi, watendaji na wanachama.
Kuwepo kwa mahitaji makubwa ya mikopo baina ya wanachama.
Kuwa na wanachama wawajibikaji.
Uwezo wa kuajiri watendaji wenye weledi.
Kuwa na wajumbe wa Bodi wenye weledi na wawajibikaji.
Uwepo wa usalama wa mali za Chama.
Uwepo wa watendaji stahiki na wenye weledi.
Imani ya bodi na watendaji kwa wanachama.