WADAU WA CHAMA

Mdau ni mtu au taasisi yeyote ambayo kwa namna moja ama nyingine anafaidika kutokana na shughuli na huduma za CHAMA.

 Chama kina wadau wafuatao;

  • Mwanachama ndiye MMILIKI wa SACCOS

  • Watendaji wapo chini ya Meneja katika;

    • Idara ya Fedha

    • Idara ya Masoko

    • Idara ya Mikopo

    • CRDB

    • KCBL (CBT)

    • EXIM

    • VODACOM

    • Shirika la Floresta Tanzania

    • Moshi Co-operative University (MoCU)

    • SCCULT (1992) LTD

    • Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO)

  • Serikali

    1. Computer Resources (T) Limited (Mifumo ya Usimamizi wa Fedha kwa SACCOS)

    2. Jikuze Business Solutions Ltd (Kampuni ya kukusanya Madeni)

    3. Higgos FPR Business Solutions Ltd (Mkaguzi wa Ndani)

Mdau 1: WANACHAMA ni akina nani?

Hawa ndio wamiliki wa Chama ambao wanapatikana kwa mujibu wa Masharti ya UVIMA SACCOS. Wanachama hutarajia huduma bora na uboreshaji wa huduma hupendekezwa na Bodi ya Chama na kupitishwa na mkutano wowote wa Chama.

Mdau 2: WATENDAJI (Wafanyakazi)

Mr. Jackson A. Mtui

Meneja na mtendaji Mkuu UVIMA SACCOS LTD

Mdau 3: Benki na Taasisi zisizo za Kifedha

Hizi ni benki za kibiashara na taasisi nyingine zisizo za kifedha ambazo Chama kinajihusisha na masuala mazima ya uwekaji na utoaji wa fedha pamoja na mikopo. Wakati wote Chama kimekuwa na Mahusiano mazuri na ushirikiano baina yake na taasisi hizi.

Mdau 4: Taasisi Mianvuli

Hizi ni baadhi ya Taasisi ambazo ni wadau wakubwa wa UVIMA SACCOS na ambao wamekua sehemu ya mafanikio ya Chama. Wadau hawa ni pamoja na;

  1. Shirika la Floresta Tanzania

  2. Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MoCU)

  3. SCCULT (1992) LTD

  4. Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO)

Shirika la Floresta Tanzania ni nini?

Floresta ni Shirika lisilo la kiserikali linalojihusisha na utunzaji wa mazingira katika Mkoa wa Kilimanjaro. Shirika hili lilianzia shughuli zake eneo la MARANGU na ndio waasisi wa UVIMA SACCOS LTD kwani historia na takwimu zinaonyesha kuwa asilimia kubwa ya wanachama anzilishi wa UVIMA walitokana na vikundi vya VICOBA vilivyokuwa chini ya Shirika hili.

Floresta imekua ikianzisha vikundi vya VICOBA hususani katika eneo lake la uendeshaji (kwa sasa shirika linafanya kazi katika wilaya za Moshi, Hai, Same, Siha na Rombo) na kuvisimamia.

Kazi muhimu zinazofanywa na Shirika hili ni kutoa na kuendesha mafunzo mbalimbali ikiwemo;

  1. Kuunda vikundi vya Ushirika wa Akiba na Mikopo

  2. Utunzaji na uhifadhi wa mazingira

  3. Mafunzo juu ya maswala ya kilimo hai ikiwemo Matumizi ya dawa asilia

  4. Maendeleo ya kiuchumi ikiwemo maswala ya ufugaji na kilimo endelevu

  5. Maswala ya huduma za kiroho kupitia kauli mbiu isemayo “Kuiponya Ardhi na Watu wake”

 

Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MoCU) ni nini?

MoCU ni Chuo cha kipekee kinachojivunia umahiri wake wa kutoa  elimu ya Ushirika ndani na hata nje ya nchi.

Chuo hiki kilianzishwa mwaka 1964 kikijulikana kama Chuo Kikuu Kishiriki cha Biashara Moshi (MUCCoBS)

Mnamo mwaka 2014 Chuo hiki kilipandishwa hadhi na kuwa Chuo Kikuu kamili kwa jina la (MoCU) kikiwa miongoni mwa Vyuo Vikuu chini ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.

Dhima ya Chuo hiki ni kutoa Elimu, Mafunzo, Utafiti na Huduma za Ushauri ili kusaidia maendeleo ya Ushirika.

Mafunzo yanayotolewa ni kwa ngazi za astashahada mpaka shahada za uzamivu kwa lengo la kupata wataalamu watakaosimamia vyema sekta hii ya Ushirika, Biashara na Asasi mbalimbali.

Kupitia MoCU, UVIMA itaendelea kutoa elimu ya Ushirika na biashara kwa wanachama na jamii ili waone fursa adhimu iliyopo ndani ya Ushirika wa Akiba na Mikopo ikiwemo UVIMA.

SCCULT (1992) Ltd ni nini?

SCCULT ni Chama Kikuu cha Ushirika wa Akiba na Mikopo Tanzania kilichoanzishwa upya mwaka 1992 kupitia Sheria ya Ushirika na. 15 ya 1991.

SCCULT ni kifupisho cha Savings and Credit Cooperative Union League of Tanzania ambacho ni Chama Mwavuli kwa Vyama vya Ushirika wa Akiba na Mikopo (SACCOS) Tanzania Bara.

Historia inayonyesha kwamba Tanzania ilikua ni nchi ya kwanza Afrika kuwa na Chama Kikuu cha Kitaifa cha Vyama vya Akiba na Mikopo.

Moja ya madhumuni ya kuwepo kwa SCCULT ni kuwakilisha SACCOS ndani na nje ya nchi na kuweka mazingira mazuri ya uendeshaji wa SACCOS ikiwa ni pamoja na kuzitetea dhidi ya taratibu na sheria zinazokwamisha maendeleo yake.

Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO) ni nini?

Mafunzo kwa watendaji wa SACCOS yaliyoendeshwa na COASCO mjini Morogoro

COASCO ni Shirika la Umma lililoanzishwa kupitia Sheria Na. 15 ya mwaka 1982 iliyofanyiwa marekebisho 2005

Lengo la kuwepo kwa COASCO ni kutoa huduma za ukaguzi wa nje (External Audit) kwa Vyama vya Ushirika ikiwemo SACCOS.

Tangu UVIMA ianzishwe 2007 imekua ikikaguliwa na COASCO kwa wakati.

Takwimu zinaonyesha kuwa, kwa ukaguzi uliofanyika kwa miaka 2 mfululizo 2022/2023 UVIMA imepata hati safi.

Mdau 4: Tume ya Maendeleo ya Ushirika (TCDC)

Serikali kupitia TCDC imekua Mdau Muhimu sana wa Ushirika (SACCOS)

Chama kinasimamiwa na Benki Kuu ya Tanzania, Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC) kama Mamlaka Kasmiwa na kwamba Chama kinatarajia kupata waraka na miongozo mbalimbali kutoka Ofisi ya Mrajis itakayosaidia uendeshaji wa shuguli za Chama.

Abdulmajid M. Nsekela

Mwenyekiti wa Kamisheni ya Tume ya Maendeleo ya Ushirika

Dkt. Benson O. Ndiege

Mrajis wa Vyama vya Ushirika na Mtendaji Mkuu Tume ya Maendeleo ya Ushirika

Utangulizi

  • Sheria ya Vyama vya Usirika Na. 6 ya 2013 sehemu ya tatu inaitambua TCDC kama Mdau muhimu sana anaehusiana na SACCOS.

  • Lengo Kuu likiwa; Uhamasishaji, usimamizi na udhibiti wa Vyama vya Ushirika

  • Tume inaundwa na Idara inayojitegemea ya Serikali ndani ya Wizara yenye dhamana ya Maendeleo ya Ushirika (Kifungu Na. 6)

  • Tume ina Bodi yenye wajumbe 11 kati ya hao 8 hutoka Asasi za Ushirika na 3 Serikalini (Kifungu Na. 7)

  • Uongozi unajumuisha; Mrajis, Manaibu Warajis na Warajis Wasaidizi.

 

Muundo wa Tume (TCDC)

Sheria ya Ushirika Na. 6 ya 2013 sehemu ya tatu (Kifungu 9), kinaeleza kuwa;

  • Tume inatakiwa kuongozwa na Mwenyekiti, Wajumbe wa Bodi, Mtendaji Mkuu (Mrajis).

  • Chini ya Mrajis kutakua na divisheni mbili (2) na sehemu sita (6) za uhamasishaji, utafiti na mafunzo, masoko, usajili, ukaguzi na usimamizi wa Vyama vya Akiba na Mikopo

  • Aidha, kutakuwa na Ofisi za Kanda ambazo zitakuwa na Warajis Wasaidizi na Maafisa Ushirika.

  • Maafisa Ushirika watakuwa chini ya Sekretariet za Mikoa & Serikali za Mitaa.

Mdau 5: Wasambazaji (Watoa Huduma)

Hizi ni taasisi ama watu ambao wanasambaza vifaa ama kutoa huduma fulani kwenye Chama. Chama kimeendelea kuwa na mahusiano mazuri baina yake na watoa huduma ili kufikia malengo ya Chama.

Mtoa Huduma 1


  • Mkurugenzi : Simeon Mitiambo - 0756 144 547

    Computer Resources (T) Limited ni Kampuni iliyoanzishwa na kusajiliwa chini ya Msajili wa Makampuni mwaka 2006 ambapo ofisi zake zipo Arusha Tanzania.

    Kampuni hii inakibali cha kutoa huduma za Mifumo ya Usimamizi wa fedha kwa SACCOS ambapo kibali hiki hutolewa na Tume ya Maendeleo ya Ushirika.

    Kampuni hii ilianza kufanya kazi na UVIMA SACCOS kuanzia mwaka 2020

    Baadhi ya bidhaa/huduma zinazotolewa na Computer Resources (T) Limited kwa taasisi na wateja binafsini ni pamoja na;

    1. SACCOS Microfinance System (Mfumo wa Huduma Ndogo za Fedha kwa SACCOS)

    2. Payroll System (Mfumo wa Malipo)

    3. Car Tracking System (Mfumo wa Ufuatiliaji wa Magari

    4. School Management System (Mfumo wa Usimamizi wa Shule)

    5. Inventory Management System (Mfumo wa Kusimamia Mali)

    6. Software Consultancy & Servicing (Ushauri wa Program una Huduma

Mtoa Huduma 2

Kampuni ya ukusanyaji wa Madeni

  • Mkurugenzi na Mtendaji Mkuu : Jesse John - 0627 616 227

    Jikuze ni kampuni inayohusika na ukusanyaji wa madeni sugu kwa Vyama vya Ushirika (SACCOS)

    Kampuni hii iliyosajiliwa 2017 ilianza kufanya kazi na UVIMA mnamo mwaka 2018 na makao yake makuu yapo mkoani Kilimanjaro.

    Hawa ni mabingwa wa ukusanyaji wa madeni katika SACCOS nchini Tanzania ambapo wanakibali cha kutoa huduma katika Mikoa 8 ikiwemo Kilimanjaro, Arusha, Manyara, Tanga, Dar es Salaam, Morogoro, Mwanza na Mbeya.

Mtoa Huduma 3


  • Meneja Kanda ya Kaskazini : Peter Mkumbo - 0752 744 457

    Higgos FPR Business Solutions Ltd ni Kampuni inayotoa huduma za ukaguzi wa ndani dhidi ya Vyama vya Ushirika (SACCOS) ndai ya nchi ya Tanzani kupitia kibali namba 142346486 ambapo kibali hiki hutolewa na Tume ya Maendeleo ya Ushirika.

    Kampuni hii ilianza kufanya kazi na UVIMA SACCOS kuanzia mwaka 2020