WAJIBU WA MWANACHAMA

1. Kukamilisha kununua hisa na kuweka akiba kwa kuzingatia Masharti ya chama.

2. Kufuata na kutekeleza Sheria na Kanuni za Vyama vya Ushirika, Masharti ya chama,

maamuzi ya Mkutano Mkuu na maelekezo mengine halali kwa mujibu wa Sheria za nchi.

3. Kurejesha mkopo kwa wakati uliopangwa;

4. Kutoa michango mbalimbali katika kuendeleza madhumuni ya chama kadri

itakavyoamuliwa na Mkutano Mkuu;

5. Kubeba dhamana endapo janga lolote litakipata chama;

6. Kuwa mwaminifu na kuonesha ushirikiano katika kutekeleza shughuli za chama;

7. Kumdhamini mkopo mwanachama mwenzake

8. Kuhudhuria semina na mafunzo yanayotolewa na Chama.

Wajibu mwingine ni Kuteua Mrithi

1. Mwanachama atamteua mrithi wake ambaye atakuwa na haki ya kulipwa hisa au maslahi

mengine katika Chama.

2. Mwanachama atakuwa na haki ya kubadilisha jina la mrithi.