Sifa za Mwanachama

Mtu yeyote anaweza kuwa mwanachama endapo atakidhi mahitaji ya Fungamano la pamoja la

uanachama na sharti awe na sifa zifuatazo: -

1. Umri wa miaka isiyopungua 18

2. Awe mwanachama wa vikundi vya VICOBA au Kijasiriamali vilivyojisajili chamani au mtu

binafsi na anayepatikana ndani ya wilaya ya Moshi.

3. Awe na uwezo wa kulipa kiingilio, hisa za uanachama na kuweka akiba kwa kiwango

kilichowekwa kwa mujibu wa masharti ya chama na awe tayari kushiriki kikamilifu shughuli

za chama.

4. Asiwe na shughuli yeyote ile inayofanana na kuweka au kukopesha wanachama ili kuondoa

mgongano wa masilahi.

5. Awe wa kuaminika na anayefahamika na wenzake/jamii